Genesis 22

Kujua Uthabiti Wa Abrahamu

1 aBaadaye Mungu akamjaribu Abrahamu. Akamwambia, “Abrahamu!”

Abrahamu akajibu, “Mimi hapa.”

2 bKisha Mungu akamwambia, “Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, Isaki umpendaye, uende katika nchi ya Moria. Mtoe huko kama sadaka ya kuteketezwa juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.”

3 cAbrahamu akaamka asubuhi na mapema siku iliyofuata, akamtayarisha punda wake. Akawachukua watumishi wake wawili pamoja na Isaki mwanawe. Baada ya kuchanja kuni za kutosha kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka kuelekea mahali Mungu alipokuwa amemwambia. 4Siku ya tatu Abrahamu akainua macho, akapaona mahali pale kwa mbali. 5 dAkawaambia watumishi wake, “Kaeni hapa pamoja na punda, wakati mimi na kijana tunakwenda kule. Tutakwenda kuabudu na kisha tutawarudia.”

6 eAbrahamu akachukua kuni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, akamtwika Isaki mwanawe, yeye mwenyewe akachukua moto na kisu. Walipokuwa wakienda pamoja, 7 fIsaki akanena akamwambia Abrahamu baba yake, “Baba yangu!”

Abrahamu akaitika, “Mimi hapa, mwanangu.”

Isaki akasema, “Moto na kuni zipo, Je, yuko wapi mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa?”

8 gAbrahamu akajibu, “Mwanangu, Mungu mwenyewe atajipatia mwana-kondoo kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa.” Nao hawa wawili wakaendelea mbele pamoja.

9 hWalipofika mahali pale alipokuwa ameambiwa na Mungu, Abrahamu akajenga madhabahu hapo, akaziweka kuni juu yake. Akamfunga Isaki mwanawe na akamlaza kwenye madhabahu, juu ya zile kuni. 10 iKisha akanyoosha mkono wake na akachukua kisu ili amchinje mwanawe. 11 jLakini malaika wa Bwana akamwita kutoka mbinguni, akamwambia, “Abrahamu! Abrahamu!”

Akajibu, “Mimi hapa.”

12 kAkamwambia, “Usimdhuru kijana, wala usimtendee jambo lolote. Sasa ninajua kwamba unamcha Mungu, kwa sababu hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee.”

13 lAbrahamu akainua macho yake, akaona kondoo dume amenaswa pembe zake nyuma yake katika kichaka. Akaenda akamchukua huyo kondoo dume, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe. 14 mAbrahamu akapaita mahali pale Yehova-Yire.
Yehova-Yire maana yake Bwana atatupa.
Mpaka siku ya leo inasemekana, “Katika mlima wa Bwana itapatikana.”

15 oBasi malaika wa Bwana akamwita Abrahamu kutoka mbinguni mara ya pili, 16 pakasema, “Ninaapa kwa nafsi yangu, asema Bwana, kwamba kwa sababu umefanya jambo hili na hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee, 17 qhakika nitakubariki, na nitauzidisha uzao wako kama nyota za angani na kama mchanga ulioko pwani. Wazao wako watamiliki miji ya adui zao, 18 rna kupitia uzao wako mataifa yote duniani yatabarikiwa, kwa sababu umenitii.”

19 sNdipo Abrahamu akawarudia watumishi wake, wakaondoka wakaenda wote pamoja mpaka Beer-Sheba. Abrahamu akaishi huko Beer-Sheba.

Wana Wa Nahori

20 tBaada ya muda, Abrahamu akaambiwa, “Milka pia amepata watoto, amemzalia ndugu yako Nahori wana: 21 uUsi mzaliwa wake wa kwanza, Buzi nduguye, Kemueli (baba wa Aramu), 22 vKesedi, Hazo, Pildashi, Yidlafu na Bethueli.” 23 wBethueli akamzaa Rebeka. Milka alimzalia Nahori nduguye Abrahamu hao wana wanane. 24 xSuria wake Nahori aliyeitwa Reuma pia alikuwa na wana: Teba, Gahamu, Tahashi na Maaka.

Copyright information for SwhNEN